SUDAN-JAMII-UCHUMI

Raia wa Sudan waendelea kususia shughuli za serikali

Kwenye mitandao ya kijamii, wanaharakati kutoka mashirka mbalimbali nchini Sudan wametoa wito tangu Jumapili Novemba kususia shughuli za serikali kwa muda wa siku tatu mfululizo.

Maandamano dhidi ya ongezeko la bei ya mafuta. Khartoum, Septemba 25, 2013.
Maandamano dhidi ya ongezeko la bei ya mafuta. Khartoum, Septemba 25, 2013. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Wito huu ulitolewa kutokana na uamuzi wa serikali wa kuongeza bei ya mafuta, dawa na umeme.

Hatua hii ya serikali imesababisha kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali mahitajio.

Raia wa Sudan wamerusha kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter picha za mitaa tiliyo upu mjini Khartoum na katika sehemu nyingine za nchi hiyo.

Wakati huo huo, maafisa wa usalama wa Sudan, mapema Jumatatu hii asubuhi wamekamata nakala ya magazeti binafsi ya kila siku ya Al-Ayyam na Al-Jareeda bila maelezo.

Kwa mujibu wa magazeti yote mawili, kukamatwa kwa nakala hizo inawezekana kuwa ni adhabu kwa magazeti hayo kutokana na kazi na kuchapishwa kwa habari hiyo kuhusu wito uliyotolewa na wanaharakati kutoka mashirika mbalimbali kwa raia kususia shughuli za serikali.

Usalama wa Sudan inaweka vikwazo vikali kuhusu uhuru wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na udhibiti kabla ya kuchapishwa habari yoyote.