SOMALIA-SIASA

Uchaguzi wa urais nchini Somalia waahirishwa tena

Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, mjini Addis Ababa, Januari 27, 2013
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, mjini Addis Ababa, Januari 27, 2013 Reuters/Tiksa Negeri

Nchini Somalia Tume ya Uchaguzi imetangaza kwamba uchaguzi wa urais uliokua umepangwa kufanyika siku ya Jumatano wiki hii nchini humo umeahirishwa tena kwa muda usiojulikana. Hii ni kwa mara ya pili uchaguzi wa Urais nchini Somalia unaahirishwa.

Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Somalia, Omar Mohamed Abdulle, amesem akatika mkutano na waandishi wa habari mjini Mogadishu kwamba haitawezekana uchaguzi huo kufanyika Jumatano wiki hii kama ilivyokuwa imepangwa.

Sababu kuu ni kuchelewa kwa uchaguzi wa wabunge ambao wanafaa kukutana na kumchagua ras wa taifa hilo.

"Tarehe kamili hitatangazwa hivi karibuni. Zoezi la kuwachagua wabunge litakapomalizika litafuata zoezi la kuwasajili, itakua tarehe 6 au 7 Desemba, na hapo ndipo kila mmoja atafahamu tarehe kamili ya uchaguzi," Omar Mohamed Abdulle amesema.

Hata hivyo amehakikisha kwamba uchaguzi huo unapaswa kufanyika kabla ya kuingia mwaka ujao.