GAMBIA-ADAMA BARROW-SIASA

Gambia yaingia katika ukurasa mpya

Adama Barrow wakati wa kampeni yake ya uchaguzi wa urais,Novemba 29, 2016.
Adama Barrow wakati wa kampeni yake ya uchaguzi wa urais,Novemba 29, 2016. REUTERS/Thierry Gouegnon

Siku moja baada ya kutangazwa msindi wa ushaguzi wa urais, Rais Mteule wa Gambia Adama Barrow alikutana Jumamosi Desemba 3 nyumbani kwake mjini Banjul na vyombo kadhaa vya habari vinavyozungumza Kifaransa.

Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano yake na vyombo hivyo vya habari, Bw Barrow alisema kuwa uamuzi wake wa kwanza utakuwa kuunda timu ambayo atafanya nayo kazi. Timu hiyo itaundwa na wajumbe kutoka vyama vinane vya muungano wa upinzani.

Rais Adama Barrow alisemakuwa hana wasiwasi wa kuliongoza taifa hilo dogo barani Afrika. "Tumetoka mbali na tumefanya kazi kubwa mpaka kufikia hapa. Ninawaambia washirika wangu wa karibu kwamba tunasonga mbele hatua kwa hatua. Moja ya hatua muhimu ni ile tuliyofikia jana (Ijumaa Desemba 2), lakini sikabiliwa na shinikizo lolote. Nina imani kuhusu matukio yafuatayo, " amesema Rais Mteule wa Gambia.

Bw Barrowa alisema kuwa aliambiwa na rais anayemaliza muda wake, ambaye alishindwa katika uchaguzi wa urais, Yahya Jammeh, kwamba anapendelea kubaki nchini Gambia na kuendelea kujihusisha na mifugo yake katika kijiji alikozaliwa. Tunapaswa kumuondolea mashaka, amesema Rais adama Barrow.

"Sina tatizo lolote kwa hilo. Ni Mgambia, anaweza kuishi nchini Gambia kama anataka. Ni mwananchi wa kawaida na rais wa zamani, nafasi yake ni hapa, " amesema Bw Barrow.

Akihojiwa kuhusu wafungwa wa kisiasa wanaozuiliwa jela, Bw Adama alisema kuwa yuko tayari kuwaachia huru, lakini hawezi kusema ni lini.

"Hawa ni watu ambao walipigana kwa ajili ya nchi yao: walitaka kuepo mabadiliko na kwa hali hiyo walitupwa jela. Kwa hiyo wanapaswa kushiriki katika mabadiliko waliyoyatetea, " amebaini Rais Mteule Adama Barrow.