AUSTRIA-SIASA

Van der Bellen aibuka mshindi, Hofer akubali kushindwa

Mwanamazingira Alexander Van der Bellen amepata ushindi katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Austria Jumapili hii Desemba 4, kwa mujibu wa runinga ya taifa ya Austria. Amemshinda mgombea wa chama cha FPO, Norbert Hofer, ambaye amekubali kwa haraka kushindwa kwake na kumpongeza mshindani wake kwa "ushindi" wake.

Rais mpya wa Austria Alexander Van der Bellen, Mei 23, 2016.
Rais mpya wa Austria Alexander Van der Bellen, Mei 23, 2016. REUTERS/Leonhard Foeger
Matangazo ya kibiashara

Waangalizi wamekua wakitarajia kukaribiana kwa wagombea hawa wawilii, kutokana na jinsi uchaguzi wa duru ya kwanza wa mwezi Mei ulivyokuwa, ambapo wagombea hao walishindana kwa kura chache kabla ya kura hizo kufutwa na Mahakam ya Katiba. Wapiga kura wa Austria wamekosoa utabiri uliokua umetolewa hapo awali.

Alexander Van der Bellen, mwenye umri wa miaka 72, kulingana na matokeo mapya ni rais mpya wa Austria. Kwa sasa anaongoza kwa 53.6% ya kura dhidi ya 46.4% alizopata mshindani wake, ambaye kwa haraka amekubali kushindwa. "Nampongeza Alexander Van der Bellen kwa ushindi wake na nawatolea wito wananchi wa Austria kushikamana na kufanya kazi pamoja," amesema Norbert Hofer ambaye amesema ana "masikitiko makubwa".

Alexander Van der Bellen, ambaye aliwania katika mbio hizo za urais kama mgombea binafsi, amepata kura nyingi katika maeneo mbalimbali ikilinganishwa na kura alizopata katika duru ya kwanza mwezi Mei, ambazo zilifutwa na Mahakama ya Katiba kutokana na kukiukwa kwa taratibu za zoezi la kuhesabu kura. Alexander Van der Bellen, amepata ushindi wa kura 31,000 dhidi ya msindani wake.