ITALIA-SIASA

Raia wa Italia wakataa rasimu ya marekebisho ya katiba, Matteo Renzi ajiuzulu

Matteo Renzi atangaza kujiuzulu kufuatia matokeo ya kura ya maoni ya katiba usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu Desemba 5, 2016.
Matteo Renzi atangaza kujiuzulu kufuatia matokeo ya kura ya maoni ya katiba usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu Desemba 5, 2016. REUTERS/Tony Gentile

Jumapili, Desemba 4, wananchi wa Italia walikataa kwa 70% ya ushiriki kwa kura ya maoni mageuzi ya kikatiba yaliyopendekezwa na Waziri Mkuu wa Italia, Matteo Renzi. Waziri Mkuu wa Italia alikubali ushindi wa kura ya "hapana" katika kura ya maoni iliyopigwa Jumapili hii Desemba 4 na akutangaza kuwa atawasilisha baraua yake ya kujiuzulu kwa Rais wa taifa hilo kuanzia Jumatatu hii.

Matangazo ya kibiashara

Wananchi wa Italia waliamua kuonyesha msimamamo wao kwa kukataa mageuzi ya kikatiba yaliyopendekezwa na Waziri Mkuu Matteo Renzi. Kiwango cha ushiriki kilifikia 70%.

Pendekezo la kupunguza madaraka ya Baraza la Seneti na mikoa lililotolewa na Matteo Renzi lilipatakwa shida zaidi ya 40% ya kura.

Mwaka mmoja uliyopita, Matteo Renzi aliahidi atajiuzulu kama atashindwa katika kura ya maoni. Kwa hiyo ni kweli kwamba Waziri Mkuu madarakani kwa muda wa miaka miwili sasa, alitangaza kujiuzulu kufuatia matokeo hayo ya kura ya maoni. Barua ya kujiuzulu itawasilishwa Jumatatu kwai Rais Italia Sergio Mattarella, baada ya kukutana mara ya mwisho na serikali yake. "Uzoefu wangu kama Waziri Mkuu unaishia hapa, " Matteo Renzi amesema katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni.

Akihutubia wanahabari usiku, kiongozi huyo alisema anakubali lawama kutokana na matokeo hayo, na kwamba kambi ya La, ambayo ilipinga mageuzi hayo, sasa inafaa kutoa mapendekezo ya mwelekeo kutoka sasa.

Kura ya "hapana" imeshinda kwa kiwango kikubwa. Napongeza viongozwa kambi iliyokua ikitetea kura ya "hapana" na nawatakia kazi nzuri kwa maslahi ya Italia na wananchi wa Italia, amesema matteo Renzi.

Kuraya Hapana iliungwa mkono na vyama vyenye sera za kujipendekeza kwa raia wengi.

Aidha, kura hiyo ya maamuzi ilitazamwa kama kipima joto cha hisia za kupinga mfumo wa kawaida wa utawala barani Ulaya.

Chama cha Five Star Movement, kilichoongoza kampeni hiyo kimesema kinajiandaa kutawala Italia sasa kufuatia kujiuzulu kwa Bw Renzi. Kiongozi wa kundi hilo alikuwa mchekeshaji Beppe Grillo.

"Kuanzia kesho, tutaanza kufanyia kazi serikali ya Five Star," mmoja wa viongozi wake, Luigi Di Maio, alisema.

Kiongozi wa upinzani Matteo Salvini, wa chama cha Northern League kinachowapinga wahamiaji, alitaja kura hiyo ya maamuzi kama "ushindi wa raia dhidi ya nguvu zinazodhibiti robo tatu ya dunia."