GHANA-UCHAGUZI

Uchaguzi Mkuu wafanyika Ghana

Wapiga kura wa Ghana wamepiga kura Jumatano Desemba 7 kumchagua rais wao.
Wapiga kura wa Ghana wamepiga kura Jumatano Desemba 7 kumchagua rais wao. REUTERS/Luc Gnago

Wananchi wa Ghana wmepiga kura Jumatano wiki hii, kumchagua rais mpya wa nchi hiyo. Wapiga kura Milioni 15 na laki saba wamepiga kura nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa idadi kubwa ya watu wamejitokeza sana kupiga kura katika Uchaguzi huu.

Kumbuka kuwa kuna wapaiga kura Milioni 15 na Laki saba ambao wanatarajiwa kupiga kura.

Zoezi hili lilianza vema asubuhi ya leo na vituo vya kupigia kura vilikua vinatarajiwa kufungwa ifikapo saa 11 kamili saa za Ghana

Kumbuka kuwa huu ni uchaguzi wa urais na wabunge lakini kwa upande wa kinyang'anyiro cha urais, kuna wagombea saba lakini ushindani mkali unatarajiwa kati ya rais wa sasa John Dramani Mahama wa chama tawala cha NDC na mpinzani wake Nana Akufo Addo wa chama kikuu cha upinzani cha New Patriotic.

Ni mara ya pili sasa kwa rais Mahama na Akufo Addo kumenyana katika kinyang'anyiro cha kutafuta uongozi wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Kwa kawaida kura zitaanza kuhesabiwa katika vituo vyote elfu 28 baada ya mtu wa mwisho kupiga kura na matokeo ya mwisho tutafahamu baada ya saa 48.

Mshindi wa urais ni lazima apate zaidi ya asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa.