GHANA-UCHAGUZI

Hali ya taharuki yatanda nchini Ghana, matokeo ya uchaguzi kuchelewa

Jumatano, Desemba 7, 2016. Hapa katika mji wa Kibi na katika maeneo mengine ya Ghana, wapiga kura milioni 15.7 wametakiwa kumchagua rais wao.
Jumatano, Desemba 7, 2016. Hapa katika mji wa Kibi na katika maeneo mengine ya Ghana, wapiga kura milioni 15.7 wametakiwa kumchagua rais wao. REUTERS/Luc Gnago

Tume ya Uchaguzi nchini Ghana imechelewa Alhamisi hii kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais masaa ishirini na nne baada ya kufungwa kwa vituo vya kupigia kura, na kusababisha hali ya taharuki katika nchi hiyo ambayo inajulikana kuwa ni moja ya nchi zilizostawi kidemokrasia katika Ukanda wa Afrika ya Magharibi

Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya maeneo ishirini na tano kati ya 275 nchini kote mpaka sasa yamehesabiwa na kuchunguzwa kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi na kura za wagombea wakuu katika uchaguzi huo, ambao ni Rais Mahama, anayewania muhula wa pili akiwa na umri wa miaka 58 na Bw Akufo-Addo, ambaye anagombea kwa mara ya tatu akiwa na umri wa miaka 72, zinakaribiana.

"Tume ya Uchaguzi inawahakikishia wananchi wa Ghana kwamba matokeo ya mwisho yatakuwa tayari katika kipindi cha masaa 72 yajayo," amesema msemaji wa Tume ya Uchaguzi, Eric Dzakpasu, katika mkutano na waandishi wa habari.

Kabla ya uchaguzi matokeo yalikuwa yalipangwa kutangazwa kati ya Alhamisi na Jumamosi usiku - lakini raia wameanza kukata tamaa kutokana na kusuiri kwa muda mrefu, hasa wafuasi wa chama cha NPP (New Patriotic Party) cha Nana Akufo-Addo ambao tayari wameanza kusherehekea ushindi wao mbele ya makazi ya kiongozi wao.

"Tumeshinda"

"Tumeshinda uchaguzi," amesema Bismark Agyei, mfuasi wa chama cha mwenye umri wa miaka 33. "Wanapaswa kutangaza ushindi huo."

Katika makao makuu ya kampeni ya chama cha NPP, tangazo la matokeo yasiyo rasmi kulingana na mashirika mbalimbali,yanampa Nana Akufo-Addo ushindi wa zaidi ya 53.5% ya kura dhidi ya 44.7% anazodaiwa kupata John Mahama.

Msemaji wa chama hicho, Oboshie Sai Cofie, ana uhakika kuwa kambi yake imeshinda uchaguzi

Televisheni binafsi inayotazamwa na watu wengi nchini Ghana, Joy News, kwa upande wake imehesabu kura za nusu ya maeneo 136 na inampa Bw Akufo-Addo ushindi lakini kwa asilimia ndogo (49.93% dhidi ya 48% kwa anazodaiwa kupata Bw Mahama).

Kama hakuna mgombea kati ya wawili hao atakayefikisha 50%, watajikuta wakipambana katika duru ya pili mwezi Desemba.