GAMBIA-SIASA-SHERIA

Rais Jammeh kupinga matokeo mbele ya Mahakama Kuu

Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, apinga matokeo ya uchaguzi, siku tisa baada ya uchaguzi
Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, apinga matokeo ya uchaguzi, siku tisa baada ya uchaguzi AFP PHOTO/Don Emmert

Rais wa Gambia anayemaliza muda wake Yahya Jammeh, ambaye alirejea kutangaza kushindwa kwake katika uchaguzi, atapinga matokeo ya uchaguzi mbele ya Mahakama Kuu, chama chake kilitangaza usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili Desemba 11.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyorushwa kwenye televisheni siku ya Ijumaa usiku, Bw Jammeh alionyesha nguvu zake kwa kutangaza, wiki moja baada ya kukubali matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi msindani wake, Adama Barrow, Desemba 1. Rais Yahya Jammeh amesem anafutilia mbali matokeo hayo na kudai uchuaguzi mpya ufanyike.

Kauli hii ya Bw Jammeh imezua hali ya sintofahamu nchini Gambia na kulaania na jumuiya ya kimataifa, ambayo ilimtaka akukubali kushindwa na kuachia madaraka kwa rais aliyechaguliwa.

Kauli hii iliyorushwa kwenye televisheni "ilikuwa utangulizi wa rufaa ambayo chama cha APRC kimekua kikiandaa kuwasilisha mbele ya Mahakama Kuu dhidi ya uamuzi wa wizi wa IEC" (Tume Huru ya Uchaguzi) kwa mujibu wa taarifa kutoka katika chama hicho.

Chamacha APRC kinanukuu Katiba, ambayo inasema kwamba Mahakama Kuu ndio chombo pekee chenye uwezo wakutatua migogoro juu ya matokeo ya uchaguzi.

Mgombea yeyote katika uchaguzi wa urais anaweza kutoa malalamiko yake mbele ya Mahakama Kuu ndani ya siku kumi baad ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, sawa na Desemba 12, lakini Jumatatu Desemba 12 ni siku ya likizo, na rufaa hii itapaswa kuwasilishwa Jumanne Desemba 13, kwa mujibu ya wanasheria. Hata hivyo, Mahakama Kuu haienezi idadi ya wajumbe. Majaji kadhaa watateuliwa kabla ya kushughulikia suala hilo.

Rais aliyechaguliwa, siku ya Jumamosi alimtokea wito Jammeh kukubali kushindwa, akitupilia mbali ombi lake la kufanyika kwa uchaguzi mpya na kuwataka wafuasi wake kuwa na utulivu.