DRC-MAREKANI

Marekani yazuia mali ya washirika wa karibu wa Joseph kabila

Naibu Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani na Usalama Evariste Boshab (kulia) akituhumiwa na marekani kuhatarisha taasisi na mchakato wa kidemokrasia nchini Jamhiri ya Kidemokrasia ya Congo.
Naibu Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani na Usalama Evariste Boshab (kulia) akituhumiwa na marekani kuhatarisha taasisi na mchakato wa kidemokrasia nchini Jamhiri ya Kidemokrasia ya Congo. AFP PHOTO / Junior KANNAH

Marekani iimetangaza Jumatatu hii Desemba 12 kwamba imechukua uamuzi wa kuzuia mali ya Evariste Boshab, Naibu Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani, na Kalev Mutond, mkuu wa upelelezi, ambao kwa mujibu wa marekani wanashtumiwa kuhatarisha taasisi na mchakato wa kidemokrasia nchini Jamhiri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Saa chache baada ya Umoja wa Ulaya, Marekani imetangaza Jumatatu hii Desemba 12 kuchukua vikwazo vipya dhidi ya viongozi waandamizi wa Kongo.

Wizara ya Hazina ya Marekani imetangaza katika taarifa yake kwamba itazuia mali ya Evariste Boshab, Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama, na Kalev Mutondo, Mkuu wa Idara ya upelelezi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (ANR).

Kama jenerali Gabriel Amisi Kumba, alamaarufu Tango Four, na aliyekuwa Mkuu wa polisi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jenerali John Numbi, wao wanashtumiwa na Marekani "kuhatarisha taasisi na kudhoofisha mchakato wa kidemokrasia."

Mali za watu hawa wawili ambazo ziko ni chini ya vyombo vya sheria vya Marekani zimezuiliwa na raia wa Marekani wamepigwa marufuku kufanya shughuli yoyote pamoja nao.

Watu muhimu katika utawala wa Kabila

Evariste Boshab, Naibu Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani na Usalama, anatuhumiwa na Marekani kuwa alitoa kitita cha fedha kwa wabunge kwa ajili ya kuunga mkono kuongozwa muhula wa Joseph Kabila.

"Ni mmoja wa watu muhimu katika mkakati wa kusalia madarakani kwa rais Kabila baada ya Desemba 19, 2016", Marekani imesema.

Kalev Mutond kwa upande wake, anatuhumiwa kuwa aliamuru simu za wapinzani wa kisiasa zifanyiwe udukuzi na alishiriki katika kuwakandamiza wafuasi wa upinzani wakati wa maandamano. "Kalev Mutond pia anaweza kuwa anahusiana na biashara haramu ya madini", Wizara ya Hazina ya Marekani imesema.