UFARANSA-IMF

Mkurugenzi Mkuu wa akabiliwa na kesi nchini Ufaransa

Mkurugenzi Mkuu wa IMF, Christine Lagarde, akanusha madai ya utumiaji mbaya wa fedha za serikali.
Mkurugenzi Mkuu wa IMF, Christine Lagarde, akanusha madai ya utumiaji mbaya wa fedha za serikali. REUTERS/Yuri Gripas

Kesi ya matumizi mabaya ya fedha za umma inayomkabili Mkurungemzi Mkuu wa Shirika la fedha duniani IMF Christine Lagarde inaanza leo nchini Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Bi.Lagarde amekanusha madai yanayomkabili kuwa wakati alipokuwa Waziri wa fedha, alitumia fedha za umma zaidi ya Euro Milioni 400 kumlipa tajiri Bernard Tapie, aliyekuwa mmiliki wa kampuni ya Adidas na klabu ya soka ya Olympique Marseille.

Kesi hii itasikilizwa katika Mahakama maalum jijini Paris ambayo iliundwa kusikiliza kesi dhidi ya Mawaziri wanaotuhumiwa kuhusika na kashfa mbalimbali.

Hata hivyo, Bi.Lagarde amekanusha madai hayo akisema kesi hii inalenga kumchafulia jina kwa sababu hatua aliyochukua kama Waziri wa fedha mwaka 2007, ilikuwa ni kwa maslahi ya taifa baada ya tajiri huyo kushinda kesi Mahakamani lakini wachunguzi wanasema fedha hizo huenda zilimsaidia Nicolas Sarkozy wakati wa Uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.