MLC yarudi kwenye meza ya mazungumzo
Imechapishwa:
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, mazungumzo ya kisiasa yameendelea Jumatano hii, huku chama cha MLC cha Jean-Pierre Bemba na washirika wake ambao walikatisha kushiriki kwao katika mazungumzo ya kitaifa wakirudi kwenye meza ya mazungumzo.
Muungano huu wa vyama vya upinzani wa FRC ulisema Jumanne wiki hii kwamba unajiondoa kwenye mazungumzo.
Muungano huu unabaini kwamba unawakilishwa katika mazungumzo hayo.
Lakini mashauriano yanaendelea ili kuwashawishi kurejea kwenye meza ya mazungumzo.
FRC ni muungano unaoundwa na chama cha MLC, vyama zaidi ya arobaini na mashirika ya kiraia hamsini.
Mazungumzo haya yanafanyika ikiwa imesalia wiki moja kabla ya kumalizika kwa muhula wa Rais Joseph Kabila, ambao unamalizika tarehe 20 Desemba.
Kurefushwa kwa muda wa kalenda ya uchaguzi imezua mgogoro wa kisiasa nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.