DRC-MAWASILIANO

Kinshasa yataka kufungwa kwa mitandao ya kijamii

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeyaomba makampuni yanayotoa huduma ya Intaneti mwishoni mwa wiki hii kufunga mitandao ya kijamii kuanzia Jumatatu hii Desemba 19, kwa sababu ya mpango wa upinzani wa kufanya maandamano dhidi ya kusalia madarakani kwa rais Joseph Kabila.

Mitandao ya kijamii inatazamiwa kufungwa nchini DRC, baada ya serikali kuagiza juma hili makampuni ya kutoa huduma za intaneti kufunga mitanado hiyo.
Mitandao ya kijamii inatazamiwa kufungwa nchini DRC, baada ya serikali kuagiza juma hili makampuni ya kutoa huduma za intaneti kufunga mitanado hiyo. REUTERS/Dado Ruvic/Illustration
Matangazo ya kibiashara

Makampuni kama Vodacom, Airtel na Orange, hayajasema kama yatazingatia agizo hilo lakini mmoja wa viongozi katika sekta hiyo amebaini kwamba makampuni ya kutoa huduma ya intaneti yalitia saini kwenye hati ambapo yalijikubalisha kuheshimu amri za serikali kuhusu masuala ya usalama.

Vyombo vya sheria vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vilimruhusu Joseph Kabila kubaki madarakani baada ya muhula wake kumalizika, ifikapo tarehe 19 Desemba 2016, na uchaguzi wa urais uliokua ulipangwa kufanyika mwezi uliyopita uliahirishwa hadi mwezi Aprili 2018.

Serikali ya Kinshasa iliwahi kufunga mitandao ya kijamii wakati wa maandamano ya upinzani mwezi Januari 2015 na ilijitetea kwa uamuzi huo kwa na haja ya kuepuka kuenea kwa uvumi wa kuchochoea vurugu.

Ombi jipya llilitolewa na mamlaka inayosimamia Posta na Mawasiliano nchini Congo katika barua ambayo Reuters ilifanikiwa kupata. Barua hiyo inadai kufungwa kwa muda mitandao ya Facebook, Twitter, Skype, YouTube na LinkedIn.