DRC-SIASA

Hali ya taharuki yatanda DRC

Mjini kati Kinshasa, DRC ambapo hali ya wasiwasi imeendelea kutanda.
Mjini kati Kinshasa, DRC ambapo hali ya wasiwasi imeendelea kutanda. Wikipédia

Wakati ambapo muhula wa pili wa rais joseph Kabila unamalizika Jumatatu hii, hali ya wasiwasi imetanda katika maeneo mbalimbali nchini DRC. Wakati huo huo ipinzani umetoa wito wa kufanyika kwa maandamano makubwa ili kupinga kusalia madarakani kwa rais huyo ambaye alimrithi babake, Laurent Desire Kabila baada ya kuuawa.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati ambapo katikati mwa juma lililopita serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliyaomba makampuni yanayotoa huduma ya Intaneti kufunga mitandao ya kijamii kuanzia Jumatatu hii Desemba 19, kwa sababu ya mpango wa upinzani wa kufanya maandamano dhidi ya kusalia madarakani kwa rais Joseph Kabila.

Vyombo vya sheria vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vilimruhusu Joseph Kabila kubaki madarakani baada ya muhula wake kumalizika, ifikapo tarehe 19 Desemba 2016, na uchaguzi wa urais uliokua ulipangwa kufanyika mwezi uliyopita uliahirishwa hadi mwezi Aprili 2018.

Serikali ya Kinshasa iliwahi kufunga mitandao ya kijamii wakati wa maandamano ya upinzani mwezi Januari 2015 na ilijitetea kwa uamuzi huo kwa na haja ya kuepuka kuenea kwa uvumi wa kuchochoea vurugu.

Ombi jipya llilitolewa na mamlaka inayosimamia Posta na Mawasiliano nchini Congo katika barua ambayo Reuters ilifanikiwa kupata. Barua hiyo inadai kufungwa kwa muda mitandao ya Facebook, Twitter, Skype, YouTube na LinkedIn.

Wakati huo Umoja wa Mataifa umetolea wito kwa wananchi wa wanasiasa nchini DRC kutumia busara kuiepusha nchi hiyo kutumbukia katika vurugu na machafuko makubwa.

Hayo yakijiri wanasiasa watano wa upinzani wamezuliwa jela tangu jana Jumapili mjini Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.