GAMBIA-SIASA

Upinzani wa Gambia wamuonya Yahya Jammeh

Rais wa Gambia Yahya Jammeh, katika mkutano na ujumbe wa viongozi wa Afrika katika upatanishi juu ya mgogoro uliyozuka baada ya uchaguzi wa Urais nchini Gambia, Desemba 13, 2016.
Rais wa Gambia Yahya Jammeh, katika mkutano na ujumbe wa viongozi wa Afrika katika upatanishi juu ya mgogoro uliyozuka baada ya uchaguzi wa Urais nchini Gambia, Desemba 13, 2016. REUTERS/Stringer

Upinzani nchini Gambia wasema Endapo rais anayemaliza muda wake nchini humo Yahya Jammeh atakataa kuondoka Madarakani atachukuliwa kama muasi. Yahya Jammeh alirejelea kauli yake hivi karibuni baada ya kutambua ushindi wa mshindani wake Adama barrow, na kutaka kura zirudi kuhesabiwa upya.

Matangazo ya kibiashara

Katikati mwa juma lililopita Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Afrika Magharibi, Mohamed Ibn Chambas, alisema kuwa Rais wa Gambia Yahya Jammeh anapaswa "kuwa tayari kukabidhi madaraka" ifikapo mwezi Januari mwakani.

Bw ibn Chambas alisema Umoja wa Mataifa hautaendelea kufumbia macho viongozi ambao hushindwa na kisha baadaye wanatumia nguvu kwa kuchukua madaraka.
"Upinzani ulishinda uchaguzi, ambao uliku halali" amesema Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa wa Ban Ki-moon katika Afrika ya Magharibi.

Jumanne Desemba 13 Marais wanne kutoka Afrika Magharibi walifanya ziara katika mji mkuu wa Gambia, Banjul na kujaribu kumshawishi Yahya Jammeh kukubali kushindwa katika uchaguzi wa urais na kukabidhi madaraka, bila mafanikio.

Mihula ya miaka mitano ya Bw Jammeh itamalizika Januari 19, Mohamed Ibn Chambas amesema, huku akiongeza kuwa "atakuwa tayari kukabidhi madaraka" tarehe hiyo.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ameendelea kulaani hatua ya jeshi kudhibiti Tume ya Uchaguzi na kuwafukuza wafanyakazi wote ambao kwa sasa hawawezi kwenda kazini.

Awali Ban Ki-moon alimtaka rais Jammeh kuamuru wanajeshi hao kuondoka katika tume hiyo mara moja.

Upinzani nchini Gambia umemuonya Yahya Jammeh ikiwa atakaidi kuachia ngazi, kuwa atachukuliwa kama adui wa nchi hiyo.