DRC-SAISA

Maaskofu wa DRC wataka kupatikana kwa makubaliano kabla ya Krismasi

Maaskofu wa Baraza Kuu la Maaskofu nchini Congo (Cenco) Marcel Utembi na Fridolin Ambongo, wakati wa kuanza kwa upatanishi kati ya upinzani na serikali iliyopo madarakani, Desemba 21, 2016.
Maaskofu wa Baraza Kuu la Maaskofu nchini Congo (Cenco) Marcel Utembi na Fridolin Ambongo, wakati wa kuanza kwa upatanishi kati ya upinzani na serikali iliyopo madarakani, Desemba 21, 2016. REUTERS/Thomas Mukoya

Maskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaoongoza mazungumzo ya kisiasa kati ya wanasiasa wa upinzani na wale wa serikali, wamesema wanataka mwafaka upatikane kabla ya Sikukuu ya Krismasi siku ya Jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo yalitarajiwa kurejelewa leo lakini hilo halijawezekana kutokana na maandamano yalishuhidiwa hasa jijini Kinshasa na Lubumbashi na kusabisha vifo vya watu 19 na wengine 45 kujeruhiwa kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa.

Bado hali ni ya wasiwasi lakini sio kama jana kama anavyoleza Reubens Mikindo, Naibu Katibu Mkuu chama cha UDPS cha Etienne Tshisekedi akiwa jijini Kinshasa.

Wakati hayo yakijiri, Ufaransa imesema kuwa huenda Rais Jospeh Kabila akawekewa vikwazo na Umoja kwa Ulaya kutokana na uamuzi wake wa kukataa kuondoka madarakani.

Msemaji wa serikali Stephane Le Foll amesema suala hili pia limejadiliwa katika Baraza la Mawaziri.