DRC-SIASA

Samy Badibanga atawazwa na mdororo wa kiuchumi kuibuka DRC

Waziri Mkuu mpya wa DR Congo, Samy Badibanga, katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa, Desemba 20, 2016.
Waziri Mkuu mpya wa DR Congo, Samy Badibanga, katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa, Desemba 20, 2016. REUTERS/Kenny Katombe

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), serikali ilikula kiapo Alhamisi Desemba 22 alasiri.Sherehe zilifanyika katika mazingira ya mvutano mkubwa. Waziri Mkuu mpya Samy Badibanga  ni mwanasiasa kutoka kambi ya upinzani.Uamuzi wa rais Joseph Kabila wa kusalia madarakani baada ya muhula wake kumalizika siku ya Jumatatu ulipokelewa vibaya sana na raia wengi wa Congo.

Matangazo ya kibiashara

Wakati wa hotuba yake, Samy Badibanga alisisitiza hasa juu ya hali ya uchumi wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Samy Badibanga, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ina wiki zisizozidi nne za fedha za kigeni kwa kulipia bidhaa kutoka nje, wakati ambapo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni nchi ambayo kwa kiasi kikubwa inaagiza bidhaa mbalimbali kutoka nje. Kati ya mwaka 2013 na 2016, fedha za kigeni ziada ziligawanywa kwa zaidi ya mara mbili, Waziri Mkuu amesema. Takwimu makubwa inayowatia wasiwasi viongozi katika ngazi ya juu serikalini.

Mpango wa Samy Badibanga unalenga sana juu ya mapambano dhidi ya mgogoro wa kiuchumi unaoathiri nchi hiyo. Pia alieleza tatizo la ugawaji wa fedhaa, akibaini kwamba pia tatizo la rushwa limekithiri, na kuahidi kuwafungulia mashitaka watu wanaohusika na ubadhirifu wa uchumi.

"Tutaendelea kwa kila njia kukabiliana na wale wanaohusika na ubadhirifu
wa mali ya umma, "
amesema Samy Badibanga

Waziri Mkuu wa DR Congo pia alizungumzia mshikamano wa kitaifa na mazungumzo chini ya mwamvuli wa Kanisa Katoliki kwa "hatima nzuri ya taifa hilo."

Kuhusu uchaguzi, Samy Badibanga uliahidi kuheshimiu muda uliopangwa chini ya mkataba wa ulioafikiwa tarehe 18 Oktoba 2016, yaani uchaguzi bora ni vizuri ufanyike mwezi Aprili 2018. Alifafanua kwamba maandalizi ya uchaguzi ni sababu ya serikali yake kuwepo. uchaguzi alisema unaweza kugharimu karibu Dola bilioni 2. Alieleza kiwango kikubwa cha fedha hizo kitatoka kwa wafadhili wa kjigeni, huku wengi wakitishia kujiondoa.

Waziri Mkuu wa DR Congo pia alisisitiza umuhimu wa kuheshimu haki za binadamu, na kuahidi kukomesha tabia ya kamta kamata ambayo imekithiri kwa sasa nchini humo, bila kusahau kesi za kisiasa na hatimaye kusisitiza umuhimu wa uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari.