GAMBIA-SIASA

Adama Barrow amtaka Yahya Jammeh kujiuzulu kama wakoloni mwaka 1965

Adama Barrow, mfanyabiashara aliyechaguliwa katika uchaguzi wa urais mwezi Desemba, amesema hataki kuongoza "nchi ambayo haiko katika amani."

Adama Barrow, rais mpya wa Gambia, hapa wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais mwishoni mwa mwezi Novemba.
Adama Barrow, rais mpya wa Gambia, hapa wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais mwishoni mwa mwezi Novemba. MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Yahya Jammeh alikubalika kushindwa Desemba 2 siku moja baada ya uchaguzi lakini wiki moja baadaye alikataa ushindi wa Bw Barrow, akibaini kuweko na kasorokatika zoezi la kuhesabu matokeo ya uchaguzi

Aliwasilisha rufaa mbele ya Mahakama Kuu kwa kuomba matokeo hayo yafutwe.

Tume ya Uchaguzi ilipinga madai ya Bw Jammeh na Adama Barrow amepanga kujitangaza rais Januari 19, siku ambapo Rais anayemaliza muda wake atakua amemaliza majukumu yake ya urais.

Toka uhuru, Gambia ilikua haijashuhudia zoezi la kupishana madarakni kwa amani.

Katika ujumbe ulirushwa kwenye mitandao ya kijamii, Bw Barrow amewatolea wito "wananchi wote wa Gambia wanaopenda amani kufanya kazi na kufanya maombi kwa ajili ya kupishana madarakani kwa amani kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii toka uhuru."

"Kama walowezi waliweza kukabidhi madaraka kwa njia ya amani kwa makubaliano ya matakwa ya wananchi wa Gambia, sisi, wananchi, tunapaswa kuonyesha mfano bora kwa watoto wetu," Adama Barrow ameongeza.

Raia wa Gambia wakimbilia Senegal

Maelfu ya raia wa Gambia wameanza kukimbilia katika nchi jirani ya senegal wakihofia kutokea kwa machafuko iwapo rais Yahya jammeh ataendelea kushikilia msimamo wake wa kukataa kuondoka madarakani ifikapo Januari 19, 2017.

Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Tume ya ECOWAS, Alain Marcel de Souza, alisema askari wa Senegal wako tayari uongozi wa operesheni ikihitajika kuingilia kijeshi nchini Gambia ikiwa Jammeh atakataa kukabidhi madaraka kwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Desemba 1.