DRC-BAN-SIASA-USALAMA

Ban Ki-moon azisihi pande zinazozungumza DRC kufikia muafaka

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa wito kwa wanasiasa nchin Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufikia haraka mwafaka wa kisiasa na tarehe ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu.

Baadhi ya wajumbe wa Barazala Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC (Cenco), wakikutana na wanasiasa mjini Kinshasa, Desemba 21, 2016.
Baadhi ya wajumbe wa Barazala Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC (Cenco), wakikutana na wanasiasa mjini Kinshasa, Desemba 21, 2016. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Aidha, amesema kuwa wananchi wa DRC ndio walio na uwezo wa kumchagua kiongozi wao.

Wito huu unakuja wakati huu mazungumzo yanayoongozwa Maaskofu wa Kanisa Katoliki yakitarajiwa kuendelea jijini Kinshasa.

Mbali na maswala ya Uchaguzi, hatima ya wafungwa wa kisiasa na wale waliokimbia nchi hiyo ni mojawapo ya suala tata linalopewa kipau mbele katika mazungumzo hayo.

Itakumbkwa kwamba mazungumzo hayo yanayoongozwa na Kanisa Katoliki nchini DRC yalikua yamesimamishwa kwa muda tangu juma lililopita.