Kiongozi wa UNAFEC, Gabriel Kyungu aondolewa kinga

Bango lenye picha ya kiongozi wa chama cha UNAFEC, Antoine Gabriel Kyungu Wa Kumwanza, mgombea katika uchaguzi wa rais kwa teketi ya chama hicho, Lubumbashi, Mei 29, 2015.
Bango lenye picha ya kiongozi wa chama cha UNAFEC, Antoine Gabriel Kyungu Wa Kumwanza, mgombea katika uchaguzi wa rais kwa teketi ya chama hicho, Lubumbashi, Mei 29, 2015. AFP PHOTO/FEDERICO SCOPPA

Mbunge Gabriel Kyungu ni mmoja wa wanasiasa wakuu wa upinzani, na ni kiongozi wa muungano wa Rassemblement katika mkoa wa Katanga na kiongozi wa chama cha UNAFEC. Anatuhumiwa kumtusi rais Joseph Kabila.

Matangazo ya kibiashara

Wabunge kumi na mbili walipiga kura ya mbunge huyo kuondolewa kinga huku kumi wakipiga kura ya hapana wakati wa kikao cha Bunge la mkoa wa Lubumbashi, kwa mujibu wa mmoja wa washauri wake.

Wanaharakati kumi na tisa wa shirika la kiraia la LUCHA waachiwa Jumanne hii

Wakati hayo yakijiri Gloria Sengha aliyetoweka kwa muda wa siku kumi, ameachiwa huru bila kufikishwa mahakamani. Wanaharakati wengine kumi na nane waliokamatwa katika mji wa Goma tarehe 21 Desemba wakati walipokuwa wakiandamana mbele ya makao makuu ya mkoa, wameachiwa huru kwa dhamana.

Kwa mujibu shirika la kiraia la LUCHA, wanaharakti watano bado wanazuiliwa katika mji mkuu wa Mkoa wa Kivu Kaskazini. Wanaharakati kadhaa wa shirika la kiraia la LUCHA bado hawajulikani walipo katika mji wa Kinshasa, ikiwa ni pamoja na Beni Carbone, mmoja wa viongozi wa vuguvugu la Filimbi aliyekamatwa mbele ya kituo cha kanisa Katoliki wakati ambapo alikua akiwataka Maaskofu na watu waliokua wakishiriki mazungumzo yao kuomba kuondoka kwa Joseph Kabila.

Wanaharakati wawili wa shirika la kiraia la Lucha waliokamatwa katika mji wa Mbuji Mayi walihamishiwa gerezani, waliomba kuachiwa huru kwa muda. Jibu ndani ya masaa 48.