DRC-SIASA-USALAMA

Watu 49 kuhukumiwa mjini Lubumbashi

Kesi ya watu arobaini na tisa waliokamatwa katika mji wa Lubumbashi wakati wa maandamano ya tarehe 19 na 20 Desemba ilifunguliwa Jumatatu asubuhi kwenye mahakama ya juu.

Katika mji wa Lubumbashi Mei 13, 2016 maandamano ya kumuunga mkono Moise Katumbi yatawanywa na polisi ambao walitumia mabomu ya machozi.
Katika mji wa Lubumbashi Mei 13, 2016 maandamano ya kumuunga mkono Moise Katumbi yatawanywa na polisi ambao walitumia mabomu ya machozi. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Watu hao wanashtumiwa uharibifu, uasi, wizi, ujambazi na kujiunga na makundi ya wahalifu.

Wanakabiliwa na adhabu hadi ya kifungo kifungo cha maisha.

Maandamano hayo yalifanyika baada ya kumalizika kwa muhula wa pili wa rais Joseph Kabila.

Maandamano kadhaa yalifanyika katika kipindi cha hivi karibuni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na watu kadhaa waliuawa.

Washtakiwa wa mjini Lubumbashi wanasaidiwa na wanasheria wengi.

Kwa mujibu wa mmoja wa mawakili wao, washitakiwa waliletwa mahakamani siku ya Jumatatu, siku tano baada ya kukamatwa kwao.