DRC-CENCO-SIASA

CENCO: mazungumzo yanakwenda vizuri

Wajumbe wa Baraza Kuu la Maskofu nchini DR Congo (Cenco) Marcel Utembi na Fridolin Ambongo, wakati wa kuanza kwa upatanishi kati ya upinzani na serikali iliopo madarakani, Desemba 21, 2016.
Wajumbe wa Baraza Kuu la Maskofu nchini DR Congo (Cenco) Marcel Utembi na Fridolin Ambongo, wakati wa kuanza kwa upatanishi kati ya upinzani na serikali iliopo madarakani, Desemba 21, 2016. REUTERS/Thomas Mukoya

Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini DRC linaloongoza mazungumzo ya kisiasa linasema mazungumzo yanakwenda vizuri na bado kuna mambo mawili ambayo mwafaka haujafikiwa.

Matangazo ya kibiashara

Cenco inasema licha ya mazungumzo hayo kwenda vizuri, bado kuna mambo ambayo bado yanajadiliwa.Mambo hayo ni pamoja na uteuzi wa mkuu atakayeongoza serikali ya mpito, lakini pia mabadiliko ya tume huru ya Uchaguzi CENI.

Wapinzani wa Rassemblement wanataka waziri mkuu wa serikali ya mpito atoke upande wao, wakati wajumbe wengine wanasema Samy Badibanga aliyeteuliwa hivi karibuni ni vema asalie kwenye wadhifa huo.

Hayo yakijriri vijana 10 wa kundi la LUCHA wanaoshinikiza mabadiliko ya kisiasa nchini DRC wanasema hawataacha kushinikiza ajenda yao licha ya kukamatwa na kufungwa jela.

Wakati huo huo shirika la kiraia katika mkoa wa Kivu Kaskazini limeomba Umoja wa Mataifa kuunga mkono wa wananchi wa DR Congo kwa kuheshimishwa kwa katiba ya nchi hiyo.

Kwa upande mwengine watetezi wa haki za binaadam mkoani humo wameiomba serikali kutilia maanani sheria za Congo wakiheshimu katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.