Zambia yavamiwa na viwavi

Miaka minne iliyoipita, viwavi waliteketeza mazao nchini Zambia.
Miaka minne iliyoipita, viwavi waliteketeza mazao nchini Zambia. Jodelet/Lépinay / Wikimedia CC

Rais wa Zambia Edgar Lungu, ametioa wito kwa kikosi cha jeshi la anga kusaidia kukabiliana na uvamizi wa viwavi nchini humo. Zambia ilishuhudia tukio kama hilo miaka minne iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Wadudu hawa wanateketeza mazao katika mikoa sita kati ya kumi inayounda nchi ya Zambia. Wadudu hao wana uwezo wa kuharibu mashamba yote.

Ndege za kijeshi zimeanza zoezi la kupulizia dawa za kuua wadudu katika maeneo yaliyoathirika zaidi.

Miaka minne iliyoipita, viwavi waliteketeza mazao nchini Zambia, hasa mahindi, mihogo, mtama na mchele.