CAMEROON-SIASA

Maaskofu wapendekeza utaratibu wa kupishana madarakani nchini Cameroon

Rais wa Cameroon Paul Biya akipiga kura katika mji wa Yaounde tarehe 9 Oktoba 2011.
Rais wa Cameroon Paul Biya akipiga kura katika mji wa Yaounde tarehe 9 Oktoba 2011. REUTERS/Akintunde Akinleye

Nchini Cameroon, Maaskofu wa mikoa inayozungumza lugha ya Kiingereza wametoa wito kwa ajili ya kurudi kwa shirikisho nchini humo ili kuepo na utaratibu wa kupisahana madarakani katika uongozi wa nchi kati ya ukanda unaozungumza Kiingereza na ule unayozungumza Kifaransa.

Matangazo ya kibiashara

Katika barua kuhusu machafuko kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa Cameroon iliyotumwa kwa Rais Paul Biya, Maaskofu wa mikoa inayozungumza lugha ya Kiingereza wameunga mkono pendekezo hilo.

Barua hi imetumwa baada ya mazungumzo kushindwa mara kadhaa kati ya serikali na vyama vya walimu wanaozungumza Kiingereza.

Serikali ya Cameroon inashindwa kupata ufumbuzi wa machafuko yanayoikumba mikoa inayozungumza Kiingereza.