DRC-MAZUNGUMZO-SIASA

Mazungumzo DRC: Maaskofu kuwasilisha mkataba wa makubaliano kwa Joseph Kabila

Wajumbe wa Baraza Kuu la Maskofu nchini DR Congo (Cenco), Desemba 21, 2016.
Wajumbe wa Baraza Kuu la Maskofu nchini DR Congo (Cenco), Desemba 21, 2016. REUTERS/Thomas Mukoya

Hii ni hatua ya mwisho kabla ya kusainiwa baadaye kwa makubaliano ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Alhamisi hii, Desemba 29, Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Cenco) wanatarajia kukutana na Rais Joseph Kabila ili kumkabidhi rasimu ya makubaliano ambayo yanaweza kumpelekea kuondoka madarakani baada ya mwaka mmoja.

Matangazo ya kibiashara

Hiyo itakuwa hatua ya mwisho ya kupitishwa kwa nakala ya mazungumzo toka wiki moja iliyopita.

Kwa sasa, hakuna sawala kwa Maaskofu la kupoteza muda unaosalia. Nakala iko mbioni kukamilishwa pamoja na marekebisho ya hivi karibuni ya yanayotarajiwa kuingizwa katika nakala hiyo. Kwa kusubiri kupitishwa na rais Joseph Kabila ambaye ni muhusika wa kwanza wa mkataba huu.

Kabla ya kumuona Joseph Kabila, Maaskofu walikutana na ujumbe wa muungano wa upinzani wa Rassemblement, muungano mkuu wa vyama vya kisiasa ambao mpaka sasa unapinga rais Kabila kubaki mamlakani baada ya muhula wake wa pili na wa mwishokulingana na Katiba ya DR Congo.

Lakini upande wa serikali na vyama vinavyoiunga pamoja na upinzani, wanasema wanakubaliana Alhamisi hii kuhusu mambo muhimu, wakibaini kwamba kunasalia tu maelezo machache ambayo yanaudhi, lakini huenda yakatatuliwa.

Kwa sasa linasalia suala la waziri mkuu. Serikali ya umoja wa kitaifa kutoka makubaliano ya awali na upande mmoja wa upinzani tayari imeundwa. Suala linakuja je rais Kabila atakubali kufuta serikali iliyoundwa hivi karibuni na na kuupa nafasi muungano wa upinzani wa Rassemblement kuchukua wadhifa wa waziri mkuu? Hili ni suala ambalo linatazamiwa kujadiliwa katika mazungumzo kati ya Maaskofu na rais Kabila.

Suala jingine linalozua mvutano: hatua kuwarahisishia, inaonekana haitoshi kwa upinzani. Upinzani unataka kuachiwa huru kwa wafungwa wengi wa kisiasa na kurejea nchini hasa kwa mmoja wa wagombea wake, mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga Moise Katumbi.