DRC-MAZUNGUMZO-SIASA

Mazungumzo kati ya serikali na upinzani kuendelea DRC

Ukumbi wa mkutano katika mtaa wa OUA mjini KInshasa ambapo kulikua kukifanyika mazungumzo ya kitaifa.où se tient le dialogue national.
Ukumbi wa mkutano katika mtaa wa OUA mjini KInshasa ambapo kulikua kukifanyika mazungumzo ya kitaifa.où se tient le dialogue national. RFI/Sonia Rolley

Mazungumzo ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yanarejelewa leo jijini Kinshasa. Mazungumzo ya leo yanalenga suala la kugawana madaraka kati ya serikali na upinzani lakini pia uundwaji upya wa tume huru ya Uchaguzi (CENI).

Matangazo ya kibiashara

Maaskofu wa Kanisa Katoliki wanaoongoza mazungmzo hayo wamesema asilimia "95%" ya makubaliano yamefikiwa huku kukiwa na tumaini kuwa siku ya Ijumaa makubaliano hayo yatatiwa saini na baadaye serikali ya mpito kuundwa.

Hata hivyo, kauli ya naibu mkurugenzi wa Ofisi ya Rais Joseph Kabila Bw. Jean-Pierre Kambila katika ukurasa wake wa twitter inatia utata akisema kuwa "matangazo ya uhakika wa kusainiwa kwa makubaliano siku ya ijumaa chini ya upatanishi wa Baraza Kuu la Maaskofu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Cenco) ni sehemu propaganda.

Kwa upande wa Baraza la Kuu la Maaskofu (Cenco), kusainiwa kwa makubaliano hayo ni suala la uaminifu si tu kwa Kanisa Katoliki lakini kwa wananchi wa Congo ambao wana matarajio makubwa kwa Kanisa hilo kufanikisha mwafaka.