DRC-MAZUNGUMZO-SIASA

Itifaki ya mkataba wa makubaliano kusainiwa DRC

Wajumbe wa Baraza Kuu la Maskofu nchini DR Congo (Cenco), Desemba 21, 2016.
Wajumbe wa Baraza Kuu la Maskofu nchini DR Congo (Cenco), Desemba 21, 2016. REUTERS/Thomas Mukoya

Mkataba wa mazungumzo ya kisiasa kati ya upinzani na serikali unatarajiwa kutiwa saini hivi leo Ijumaa Desemba 30 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Maaskofu wa kanisa katoliki wamekuwa wanaongoza mazungumzo haya na siku ya Alhamisi jioni walikutana na rais Joseph Kabila kuwasilisha nakala ya mkataba huo, kabla ya kutiwa saini leo jijini Kinshasa.

Maaskofu hao wamesema hawataki tena kuwepo kwa mazungumzo mengine huku wakisisitiza kuwa mambo ambayo hayakukubaliwa, yatamalizwa leo.

Maaskofu hao pia tayari wamekutana na ujumbe wa muungano wa upinzani wa Rassemblement. Sanjari na hayo pande zote mbili zimeelezea kukubaliana kwa masuala muhimu.

Kuelekea kutiwa saini kwa mkataba huu, maswali yanayoulizwa ni ikiwa rais Kabila amekubali kuondolewa kwa Waziri Mkuu wa sasa na kukubali atakayeteuliwa na Etienne tshisekedi? Na je, nini hatma ya wafungwa wa kisiasa pamoja na aliyekuwa Mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga Moise Katumbi?