ISRAEL-NETANYAHU-RUSHWA

Netanyahu akabiliwa na kashfa ya rushwa

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiri kuwa mwaka 2001, alipokea Dola za Marekani 40,000 kutoka kwa tajiri kutoka Ufaransa Arnaud Mimran.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiri kuwa mwaka 2001, alipokea Dola za Marekani 40,000 kutoka kwa tajiri kutoka Ufaransa Arnaud Mimran. REUTERS/Abir Sultan/Pool

Polisi nchini Israel wanatarajiwa kumhoji Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kuhusu madai ya kupokea zawadi kutoka kwa wafuasi, kinyume na sheria.

Matangazo ya kibiashara

Lengo la mahojiano haya ni kubaini ikiwa Netanyahu, alipokea zawadi hizo kinyume na sheria kutoka kwa matajiri wanaomuunga mkono.

Uchunguzi huu pia unalenga kubaini ikiwa Netanyahu alipokea Maelfu ya fedha kutoka kwa wafanyibiashara kutoka nje ya nchi lakini, pia Waisraeli wanaomuunga mkono.

Hata hivyo, uchunguzi huu haujathibitishwa na polisi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kupitia ukurasa wake wa facebook, Netanyahu amekanusha madai hayo na kusema kuwa maadui wake wa kisiasa wanatumia mbinu hiyo kuiangusha serikali yake.

Licha ya tuhuma hizi, Netanyahu amekiri kuwa mwaka 2001, alipokea Dola za Marekani 40,000 kutoka kwa tajiri kutoka Ufaransa Arnaud Mimran, wakati hakuwa Ofisini, fedha alizotumia kuinua sifa ya Israel nje ya nchi.