Utekelezaji wa mkataba DRC: Serikali yatoa masharti
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na vyama vinavyoiunga mkono, Jumanne hii Januari 3 vimetoa mashartikatika kushiriki kwake katika mazungumzo juu ya utekelezaji wa mkataba wa makubaliano na upinzani uliosainiwa Jumamosi Disemba 31, 2016.
Imechapishwa:
Maaskofu Katoliki waliitaka serikali na upinzani kuja Jumatano kutoa mapendekezo yao yaliyoandikwa juu ya utaratibu wa uteuzi wa Waziri Mkuu, wa wajumbe wa Baraza la kitaifa la ufuatiliaji wa mkataba na mchakato wa uchaguzi (CNSA), muundo wa serikali na kugawana madaraka katika kipindi cha mpito, kwa mujibu wa Kasisi Donatien Nshole, msemaji wa Baraza Kuu la Maaskofu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Lakini serikali na vyama vinavyoiunga mkono wametoa masharti juu ya utekelezaji wa makubaliano yaliyosainiwa Desemba 31. Kambi hii inalenga kupata ufumbuzi wa mgogoro uliosababishwa na kusalia madarakani kwa rais Joseph Kabila licha ya kumalizika kwa muda wa kipindi chake.
"Maaskofu wanapaswa kwanza kuwasilisha ripoti kuhusu mkataba kwa rais wa Jamhuri, naye atathibitisha amepokea ripoti hiyo," amesema Aubin Minaku, katibu mkuu wa muungano wa vyama vinavyoiunga mkono serikali (MP).
Minaku Aubin, ambaye pia ni Spika wa Bunge, amebainisha kuwa muungano huo hauwezi kutamka juu ya utekelezaji wa makubaliano bila kusikia ushauri mzuri wa Joseph Kabila. "Ni wakati wa kuheshimu madaraka ya Rais wa Jamhuri, Katiba na taasisi mbalimbali zaJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo," Bw Minaku amesisitiza.
"Hakuna kuchelewa, hakuna udhuru, hakuna kizuizi"
Mmoja wa wapinzani wakuu wa serikali amepinga dhidi ya hoja yoyote ya kutaka kususia maelewano ambayo yanaruhusu rais Kabila kubaki katika wadhifa huo hadi wakati wa uchaguzi, mwishoni mwa mwaka huu, na kutowania katika uchaguzi huo.
"Hakuna kuchelewa kwa makusudi, hakuna udhuru, hakuna kizuizi kitakacho vumiliwa katika utekelezaji wa makubaliano", Moise Katumbi Chapwe, mwanasiasa wa upinzania aliye uhamishoni, ameandika katika taarifa yake.