GAMBIA-SIASA

Yahya Jammeh aungwa mkono na jeshi la Gambia

Mkuu wa majeshi ya Gambia, Jeneral Ousman Badjie (hapa ilikua Desemba 13, 2016) atangaza kumuunga mkono rais Yahya Jammeh.
Mkuu wa majeshi ya Gambia, Jeneral Ousman Badjie (hapa ilikua Desemba 13, 2016) atangaza kumuunga mkono rais Yahya Jammeh. Photo: Seyllou/AFP

Mkuu wa majeshi nchini Gambia ametangaza kumuunga mkono rais wa taifa hilo Yahya Jammeh licha ya mgogoro unaondelea nchini humo, huku upinzani ukimtaka rais huyo kutothubutu kusalia madarakani ifikapo Januari 19.

Matangazo ya kibiashara

Katika barua kwa magazeti yanayounga mkono serikali, Jenerali Ousman Badjie aliahidi kwamba jeshi litamtii rais huyo.

Uingiliaji wa kati wa Jenerali Badjie unafuatia vitisho vya kijeshi vya jamii ya kiuchumi ya mataifa ya Magharibi ECOWAS iwapo Jammeh atakataa kuondoka madarakani ifikiapo Januari 19.

Rais Jammeh amesema kuwa hatua yoyote kama hiyo itasababisha vita.
Hivi karibuni kambi ya Adama Barrow aliyetangazaw mshind wa uchaguzi wa urais, lilikuwa limedai kuungwa mkono na Jenerali Badjie.

Hatua hiyo ya jeshi inaonekana kuzua hali ya sintofahamu katika kuanzisha serikali mpya baada ya Jammeh aliyekuwa madarakani kwa miaka 22.

Mapema mwezi Desemba 2016 Muungano wa wanasheria nchini Gambia ulisema kuwa kitendo cha rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh kukataa matokeo ya kura zilizoonyesha kuwa ameshindwa katika uchaguzi uliopita ni kuisaliti nchi hiyo.

Hapo awali Jammeh alikubali kushindwa na kuahidi kuondoka madarakani lakini aliyakataa matokeo ya uchaguzi siku chache baadaye.