Wanasiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC wamefikia makubaliano ya mchakato wa kipindi cha mpito kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwaka huu wa 2017 licha kuwepo changamoto mbalimbali. Je kusainiwa kwa makubaliano hayo kutaivusha DRC kutoka katika wimbi la ukosefu wa usalama na amani pamoja na mgogoro wa kisiasa? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kupata majibu ya swali hilo.