COTE D'IVOIRE-SIASA

Guillaume Soro achaguliwa tena kuwa Spika wa Bunge nchini Cote d'Ivoire

Waziri mkuu wa zamani wa Cote d'Ivoire, Guillaume Soro Kigbafori, amechaguliwa tena Jumatatu hii Januari 9 kwa awamu ya pili kuwa Spika wa Bungela nchi hiyo, masaa machache baada ya kujiuzulu kwa serikali na Waziri Mkuu, Daniel Kablan Duncan.

Waziri mkuu wa zamani wa Cote d'Ivoire ,Guillaume Soro, achaguliwa kuwa Spika wa Bunge  wa nchi hiyo.
Waziri mkuu wa zamani wa Cote d'Ivoire ,Guillaume Soro, achaguliwa kuwa Spika wa Bunge wa nchi hiyo. Reuters/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Guillaume Soro mwenye umri wa miaka 44, aliyekuwa Waziri Mkuu na kiongozi wa zamani wa kundi la waasi la New Forces, amepata kura 230 kwa jumla ya kura 252, sawa na zaidi ya 95% ya kura zilizopigwa.

Guillaume Soro alikua akishindana na Evariste Méambly, Mbunge wa chama cha PDCI kutoka Facobly, aliyewania kama mgombea binafsil. Amepata kura 12 kura. Kwa jumla ya kura 252 kura.

Alassane Ouattra Jumanne asubuhi atarajiwa Bungeni

Dakika chache baada ya kuchaguliwa kwake, Guillaume Soro amekaribisha ushindi wake klwa matokeo hayo, na kutoa "shukrani" zake kwa rais Alassane Ouattara na kwa Henri Konan Bedie.

Soro pia amethibitisha kwamba Alassane Ouattara atalihutubia Bunge hii Jumanne asubuhi saa 4:00 saa za Afrika ya Magharibi. Kwa vyanzo vilivyo karibu ya ofisi ya rais, rais Ouattara atamteua Makamu wake wakati wa hotuba hiyo kwa Wabunge.