COTE D'IVOIRE-SIASA

Amadou Gon Coulibaly ateuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Cote d'Ivoire

Katibu mkuu wa Ofisi ya rais nchini Cote d'Ivoire, Amadou Gon Coulibaly, ateuliwa na  Alassane Ouattara kwenye nafasi ya waziri Mkuu, Januri 10, 2017.
Katibu mkuu wa Ofisi ya rais nchini Cote d'Ivoire, Amadou Gon Coulibaly, ateuliwa na Alassane Ouattara kwenye nafasi ya waziri Mkuu, Januri 10, 2017. REUTERS/Thierry Gouegnon

Amadou Gon Coulibaly ameteuliwa Jumanne hii Januari 10 kuwa Waziri Mkuu wa Cote d'Ivoire. Anachukua na nafasi ya Daniel Kablan Duncan, ambaye mapema asubuhi aliteuliwa na rais Alassane Ouattara kwenye nafasi ya Makamu wa rais.

Matangazo ya kibiashara

Amadou Gon Coulibaly, mwenye umri wa miaka 57, awali alikua Waziri wa Nchi na Katibu mkuu wa Ofisi ya rais. Ameombwa na rais wa nchi hiyo "kuunda serikali mpya haraka iwezekanavyo."

Amadou Gon Coulibaly ni mshirika wa karibu wa Alassane Ouattara, Mbunge wa jimbo la Korhogo ambaye alitangaza mwezi Januari mwaka 2012 katika gazeti la Jeune Afrique kuhusu rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara "rais Ouattara ndiye ambaye alinifunza mengi kuhusu siasa, katika kazi yangu nitakua pamoja naye siku zote, " alisema Bw Coulibaly.

Uteuzi wake unakuja saa chache baada ya kujiuzulu kwa Daniel Kablan Duncan kwenye nafasi ya Wazir Mkuu na kuteuliwa kwake kwenye nafasi ya makamu wa rais, tangazo ambalo limlikua likisubiriwa, na kutolewa na rais Alassane Ouattara Jumanne hii asubuhimbele ya Bunge la taifa. Siku moja kabla, aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa jimbo la Grand-Bassam alitangaza kujiuzulu kwake na kujiuzulu kwa serikali yake.