MAREKANI-SIASA-OBAMA

Barack Obama: leo Marekani ni bora zaidi na yenye nguvu

Barack Obama alitoa hotuba yake ya kuaga katika mji wa Chicago, Januari 10, 2017.
Barack Obama alitoa hotuba yake ya kuaga katika mji wa Chicago, Januari 10, 2017. REUTERS/John Gress

Siku chache kabla ya kukabidhi madaraka, rais wa Marekani Barack Obama, katika hotuba yake aliyoitoa Jumanne wiki hii amezungumzia kazi kubwa alioifanya katika kipindi cha miaka minane aliongoza Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Marekani ni nchi "bora zaidi na yenye nguvu" alisema Barack Obama Jumanne hii jioni katika mji wa Chicago. Wakati wa hotuba hiyo ya mwisho kama rais, alisisitiza mafanikio yaliyofikiwa. Akitoa mfano wa ajira, bima ya afya, ndoa kwa wote, mahusiuano na Cuba, makubalianokuhusu mpango wa nyuklia wa Iran au kifo cha Osama Bin Laden.

Hata hivyo rais Barack Obama alitambua kwamba suala la rangi bado ni changa moto kubwa "linalosababisha mgawanyiko" nchini Marekani. Alisema kuwa uhamiaji ni nguvu ya Marekani. "Ninafutilia mbali ubaguzi dhidi ya Waislamu Wamarekani," alisema rais Obama.

Rais Obama ndiye rais wa kwanza nchini Marekani wa asili ya Afrika na alichaguliwa mwaka 2008 akiahidi kurejesha matumaini na kutekeleza mabadiliko.
Mrithi wake Donald Trump aliahidi kubatilisha baadhi ya sera kuu alizofanikisha Bw Obama.

Timu yake ilisema kuwa asingeweza kushambulia mrithi wake. Kama Donald Trump hakutajwa kwa majina yake, watu waliohudhuria mkutano wa hadhara katika mji wa McCormick walimuona rais huyo mteule wa Marekani kwa kauli alizokua akitoa dhidi ya Waislamu. Rais Barack Obama alisema kuwa kukanusha mabadiliko ya tabia nchi ni "kusaliti vizazi vijavyo."

Kumekuwa na majadiliano mengi ya umoja na demokrasia, neno lililotamkwa sana kwa muda wa dakika hamsini za hotuba hiyo. Rais Barack Obama amewahimiza Wamarekani kuitetea demokrasia.

"Kwa kila kipimo, Marekani sasa ni bora zaidi, na ina nguvu zaidi" kuliko ilivyokuwa miaka minane iliyopita alipochukua madaraka, amewaambia maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika mjini humo.

Hata hivyo, "demokrasia inatishiwa kila inapokosa kutiliwa maanani," alisema rais Obama.

Amewaomba Wamarekani wa kila asili kuangazia mambo kutoka kwa msimamo wa wengine, na kusema kwamba "lazima tuwategee sikio wengine na kusikia".