Gurudumu la Uchumi
Rais Obama amefanikiwa kiasi gani kuisaidia nchi yake na bara la Afrika kiuchumi
Imechapishwa:
Cheza - 09:52
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili inaangazia hotuba ya mwisho ya rais wa Marekani Barack Obama, aliyoitoa usiku wa kuamkia Jumatano ya Januari 11 barani Afrika, ambapo kubwa ni sera yake ya ushirikiano wa kimataifa na hasa kiuchumi na nchi za Afrika na mustakabali wa baadae wa Marekani baada ya rais mteule Donald Trump kuchukua madaraka rasmi.Mtangazaji wa makala haya, amezungumza na mchambuzi wa masuala ya uchumi, Dr Wetengere Kitojo, kutathmini ni kwa kiasi gani rais Obama amefanikiwa na sera yake ya kimataifa kuhusu uchumi na biashara.