GAMBIA-SIASA

Mahakama ya juu yashindwa kuchukua uamuzi kuhusu kuapishwa kwa Adama Barrow

Mmoja wa Majaji katika Mahakama ya Juu nchini Gambia, amejiondoa katika kesi iliyowasilishwa na rais Yahya Jammeh akitaka Mahakama kuzuia kisheria kuapishw kwa Adama Barrow siku ya Alhamisi.

Adama Barrow, rais mteule wa Gambia, hapa wakati wa kampeni ya uchaguzi wa urais mwishoni mwa mwezi Novemba 2016.
Adama Barrow, rais mteule wa Gambia, hapa wakati wa kampeni ya uchaguzi wa urais mwishoni mwa mwezi Novemba 2016. MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hili linaonekana pigo kubwa kwa rais Jammeh, baada ya Mahakama hiyo kuahirisha pia kusikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Barrow, kutokana na ukosefu wa Majaji wa kusikiliza kesi hiyo.

Hayo yanajiri wakati ambapo Adama Barrow aliyeshinda katika uchaguzi wa urais nchini Gambia, kwa sasa anaendelea akuishi kwa muda nchini Senegal, kwa mujibu wa serikjali ya Senegal.

Hivi karibuni msemaji wa rais mteule wa Gambia Adama Barrow alisema, sherehe ya kumwapisha zitaendelea kama zilivyopangwa siku ya Alhamisi juma hilli jijini Bunjul.
Hakikisho hili linakuja wakati huu Barrow akiwa nchini jirani ya Senegal, atakakokuwa hadi kuapishwa kwake.

Hatua ya Barrow, kwenda Senegal ilischukuliwa na viongozi wa Afrika Magharibi ECOWAS waliokutana nchini Mali mwishoni mwa juma, baada ya rais Yahya Jammeh kuendelea kukataa kuondoka madarakani.

Ripoti kutoka chini Senegal zinasema kuwa rais mteule wa Gambia Adama Barrow atasalia nchini Senegal hadi wakati wa kuapishwa kwake wakati huu ambapo nchi ya Gambia inakumbwa na mzozo wa kisiasa ulizuka baada ya rais Yahya Jammeh kukataa kuachia ngazi.

Vyombo vy habari nchini Senegal vimearifu kwamba rais wa Senegal Macky Sall, amekubali kumpa makao bwana Barrow katika mji mkuu Dakar hadi hadi Januari 19 siku ambayo atakapoapishwa na kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi ya Gambia.

Jumamosi Januari 14, rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, alimtaka rais wa Gambia kuachia ngazi ifikapo tarehe 19 Januari ili kuzuia umwagaji damu.

Rais Yahya Jammeh ameendelea kukataa kukubali kuwa alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Desemba na kusema bado anasubiri uamuzi wa mahakama ya juu kuhusu madai aliyowasilisha kwa mahakama hiyo, ambayo hivi karibuni iliahirish akusikiliza kesi hiyo hadi mwezi Mei mwaka 2017.