UFARANSA-SIASA-VALLS

Manuel Valls apigwa kofi na mpita njia katika mji wa Brittany

Ikiwa si chini ya mwezi mmoja baada yakurushiwa unga katika mji wa Strasbourg, Manuel Valls, Jumanne hii, Januari 17alipigwa kofi na mpita wakati wa ziara yake katika eneo la Lamballe mjini Brittany, alipokua akihamasisha katika kampeni za chama cha Kisoshalisti katika Uchaguzi mkuu wa urais nchini Ufarans

Manuel Valls, katika mji wa Villeurbanne Januari 17, 2017.
Manuel Valls, katika mji wa Villeurbanne Januari 17, 2017. REUTERS/Robert Pratta
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea wakati alipokua akitokea katika eneo la Lamballe, mjini Brittany. Manuel Valls aliandamana na Waziri wa Ulinzi Jean-Yves Le Drian, ambaye alikuja kumuunga mkono katika kampeni yake kwa kura za mchujo za chama cha Kisoshalisti.

Alipokuwa akihutubia katika ukanda wa Magharibi mwa mji wa Brittany alipigwa kofi na kijana mdogo alipokuwa akisalimia kwa kushikana mikono.

Manuel Valls, wakati huo huo, iliendelea na kampeni yake. Alipoulizwa kuhusu yaliyotokea, alijibu dakika chache baadaye, akisema kuwa "kuna wale ambao wanapinga demokrasia na wale ambao wanaminya demokrasia, hao ni wanasiasa. Kama nimejikubalisha kuingia katika kinyang'anyiro hiki, ni kwa sababu sina hofu ya mawasiliano na mahusiano na wananchi wenzangu, licha ya maoni yao. Lakini najua kwamba demokrasia, sio vurugu. Na mtu ambaye anampiga kofi mwanasiasa, ni jambo baya kabisa, lakini mimi sijali hayo, nataka kuwashawishi wananchi wa Ufaransa, " amesema Manuel Valls.