Gurudumu la Uchumi

Seheumu 1: Utandawazi umeleta mabadiliko ya kiuchumi au unaendelea kubomoa

Sauti 08:45
Polisi wa Uswis akifanya doria juu ya dari la jumba la mikutano la kimataifa mjini Davos unakofanyika mkutano wa kiuchumi wa World Economic Forum, Januari 17, 2017.
Polisi wa Uswis akifanya doria juu ya dari la jumba la mikutano la kimataifa mjini Davos unakofanyika mkutano wa kiuchumi wa World Economic Forum, Januari 17, 2017. REUTERS/Ruben Sprich

Mtangazaji wa makala haya, juma hili amezungumza na wataalamu wa masuala ya uchumi, katika sehemu ya kwanza ya mjadala kuhusu "Utandawazi", na swali la msingi ni je, Utandawazi umesaidia kuimarisha uchumi wa dunia, ama ni wachache tu wanaonufaika na maendeleo ya utandawazi? Ungana na mtayarishaji wa makala haya akizungumza na Profesa Hamfrey Moshi na Dr Wetengere Kitojo.