GAMBIA-SENEGAL-GAMBIA-USALAMA

Vikosi vya Senegal njiani kuelekea Gambia

Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Umma wa majeshi ya Senegal (DIRPA) ameiambia BBC kuwa mipango ya shughuli za kuingilia kijeshi imeanza.

Senegal iliteuliwa na ECOWAS ili kuongoza operesheni ya kuingilia kijeshi dhidi Rais Yahya Jammeh.
Senegal iliteuliwa na ECOWAS ili kuongoza operesheni ya kuingilia kijeshi dhidi Rais Yahya Jammeh. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Jenerali François Ndiaye, Mkuu wa jeshi la ardhini ndiye ataongoza askari wa Senegal," amesema Bw Ndiaye, mkurugenzi wa DIRPA.

Mwandishi wa habari wa Senegal ambaye anaishi katika mji wa Ziguinchor amesema kuwa askari wa Senegal wamewasili katika bandari ya Ziguinchor, kusini mwa Senegal.

Senegal iliteuliwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kuongoza operesheni ya kuingilia kijeshi nchini Gambia kumuondoa madarakani rais anayemaliza muda wake yahya Jammeh ambaye amekataa kuachia madaraka baada ya kushindwa Desemba 1.

Aidha, viongozi tawala katika manispaa ya jiji la Djouloulou katika mkoa huo wa kusini mwa Senegal, kilomita kumi na tano na mpaka wa Gambia, amewatolea wito viongozi wa Senegal na mashirika yasiyo ya kiserikali kusaidia kuwahudumia maelfu ya watu ambao waliikimbia nchi ya Gambia na katika mji huo.

Kwa mujibu wa Katibu wa manispaa ya jiji la Diouloulou, Amadou Oury Diallo, toka kushindwa kwa rais anayemaliza muda wake Yayah Jameh katika uchaguzi wa urais wa Desemba 1, Djouloulou imewapokea karibu watu 800 ambao wanawasili na kiwango kidogo cha chakula na mavazi.

Wakati huo huo katikamji wa Banjul hali ya wasiwasi imetanda ikiwa zimesalia tu saa chache ili kukamilika kwa muda wa kuongoza kwa muhula wa Rais Yahya Jammeh.

Mitaa imebaki patupu wakati ambapo watalii kutoka mataifa ya mataifa mbalimbali wameondoka nchini humo.