MAREKANI-TRUMP-SIASA

Donald Trump kuapishwa Ijumaa kama rais mpya wa Marekani

Marekani inaelekea kupata rais mpya. Donald Trump ataapishwa siku ya Ijumaa Januari 20 jijini Washingtin DC, nchini Marekani kama rais wa 45 wa Marekani

Kutakuwa na msafara baada ya sherehe ya kuapishwa ambao utaanza katika vidato vya jumba la Capitol Building kuelekea ikulu ya White House kupitia barabara maarufu ya Pennsylvania Avenue.
Kutakuwa na msafara baada ya sherehe ya kuapishwa ambao utaanza katika vidato vya jumba la Capitol Building kuelekea ikulu ya White House kupitia barabara maarufu ya Pennsylvania Avenue. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Rais Barack Obama anayemaliza muda wake akizungumza na wanahabari kwa mara ya mwisho kabla ya kuondoka madarakani, alimtaka Trump kuhakikisha kuwa anatofautisha maswala ya vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi na maswala ya silaha za Nyuklia.

Bw Trump aliyeshinda uchaguzi wa urais wa tiketi ya chama cha Republican anatarajiwa kuapishwa mbele ya watu 750,000 mbele ya majengo makuu ya bunge la Marekani, Capitol Building, Washington D.C.

Miaka minane iliyopita, Rais Obama alipokuwa anaapishwa kuwarais, watu 1.8 milioni walihudhuria sherehe hiyo.

Kisheria, rais anafaa kuapishwa kabla ya saa sita mchana saa za Amerika Mashariki ambazo Afrika Mashariki ni saa mbili usiku.

Wanamuziki walioalikwa wataanza kutumbuiza saa kumi na moja na nusu jioni (Saa za Afrika Mashariki).

Hotuba za kufungua sherehe zitaanza kutolewa saa moja na nusu usiku.

Muda mfupi kabla ya saa Mbili usiku saa za Afrika Mashariki, Donald Trump atalishwa kiapo cha kuwa rais wa Marekani na Jaji wa Mahakama ya Juu John Roberts.

Baadaye, kutakuwa na msafara baada ya sherehe ya kuapishwa ambao utaanza katika vidato vya jumba la Capitol Building kuelekea ikulu ya White House kupitia barabara maarufu ya Pennsylvania Avenue.

Ikulu ya White House, Januari 15, 2017, siku chache tu kabla ya kuapishwa kwa Donald Trump.
Ikulu ya White House, Januari 15, 2017, siku chache tu kabla ya kuapishwa kwa Donald Trump. REUTERS/Carlos Barria

Bw Trump na mkewe Melania baadaye watacheza densi katika matamasha matatu, mawili katika ukumbi wa mikutano wa Walter E Washington na jingine katika ukumbi wa Jengo la Makumbusho ya Taifa.

Miaka minane iliyopita, Rais Obama alipokuwa anaapishwa kuwarais, watu 1.8 milioni walihudhuria sherehe hiyo.

Inaarifiwa kuwa siku moja baada ya kuapishwa kwa Bw Trump, wanawake takriban 200,000 wanatarajiwa kuandamana Washington DC na miji mingine kumpinga Bw Donald Trump.