Kutawazwa kwa Donald Trump: Sherehe zaanza mjini Washington
Imechapishwa:
Donald Trump amewasili Alhamisi hii, Januari 19 mjini Washington. Ameletwa na ndege ya kijeshi ambako ataapishwa siku ya Ijumaa kuwa rais wa 45 wa Marekani. Sherehe tayari zimeanza mjini Washington.
Bw Trump aliyeshinda uchaguzi wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican anatarajiwa kuapishwa mbele ya watu 750,000 mbele ya majengo makuu ya bunge la Marekani, Capitol Building, Washington D.C.
Miaka minane iliyopita, Rais Obama alipokuwa anaapishwa kuwarais, watu 1.8 milioni walihudhuria sherehe hiyo.
Kisheria, rais anafaa kuapishwa kabla ya saa sita mchana saa za Amerika Mashariki ambazo Afrika Mashariki ni saa mbili usiku.
Wanamuziki walioalikwa wataanza kutumbuiza saa kumi na moja na nusu jioni (Saa za Afrika Mashariki).
Hotuba za kufungua sherehe zitaanza kutolewa saa moja na nusu usiku.
Muda mfupi kabla ya saa Mbili usiku saa za Afrika Mashariki, Donald Trump atalishwa kiapo cha kuwa rais wa Marekani na Jaji wa Mahakama ya Juu John Roberts.
Baadaye, kutakuwa na msafara baada ya sherehe ya kuapishwa ambao utaanza katika vidato vya jumba la Capitol Building kuelekea ikulu ya White House kupitia barabara maarufu ya Pennsylvania Avenue.
Bw Trump na mkewe Melania baadaye watacheza densi katika matamasha matatu, mawili katika ukumbi wa mikutano wa Walter E Washington na jingine katika ukumbi wa Jengo la Makumbusho ya Taifa.
Miaka minane iliyopita, Rais Obama alipokuwa anaapishwa kuwa rais, watu 1.8 milioni walihudhuria sherehe hiyo.
Inaarifiwa kuwa siku moja baada ya kuapishwa kwa Bw Trump, wanawake takriban 200,000 wanatarajiwa kuandamana Washington DC na miji mingine kumpinga Bw Donald Trump.