MAREKANI-TRUMP-SIASA

Donald Trump aahadi kuirejeshea Marekani hadhi yake

Katika hotuba yake, Donald Trump ameahadi, kama katika kampeni yake ya uchaguzi "kuifanya Marekani kuwa ni nchi yenye nguvu zaidi. "
Katika hotuba yake, Donald Trump ameahadi, kama katika kampeni yake ya uchaguzi "kuifanya Marekani kuwa ni nchi yenye nguvu zaidi. " AFP/Drew Angerer/Getty Images

Donald Trump ameapishwa leo Ijumaa, Januari 20 kama rais 45 wa Marekani katika sherehe iliofanyika katika majengo makuu ya Bunge la Congress, Capitol Hill saa 05:46 saa za Washington (sawa na saa 01:46 jioni saa za Afrika ya Mashariki).

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kufyatua mizinga 21 hewani, Donald Trump alitoa hotuba yake ya kwanza kama rais. Donald Trump ameahadi kuwapa nafasi kubwa wananchi wa Marekani katika madaraka, akisema kuwa wamewasahau kwa muda mrefu sana. "Siku hii ya leo ni yenu na Marekani ni nchi yenu," amesema Obama.

Akiweka mkono wake wa kushoto juu ya Biblia mbili, huku akiinua mkono wake wa kulia, Donald Trump amekula kiapo mbele ya Rais wa Mahakama Kuu John G. Roberts Jr. Na kuwa rasmi rais wa 45 wa Marekani.

Donald Trump ametoa kanuni mbili ambazo zitaongoza sera yake ya siasa "kununua vifaa vya Marekani, kuajiri Mmarekani."

Katika hotuba yake, Donald Trump amesema anajutia kuona Marekani ilitajirisha nchi za nje kwa gharama za Marekani. "Hayo yameshapita," Trump amesema. "Tangu siku hii ya leo, Marekani itapewa kipaumbele sawa na suala la biashara, viwanda, au uhamiaji", amebaini Bw Trump.

Donald Trump amehadi kuimarisha ushirikiano wa zamani na kujenga ushirikiano mpya. "Ugaidi wa Waislamu wenye msimamo mkali utatokomezwa," Bw Trump Ameonya.

Donald Trump, alimaliza hotuba yake kwa maneno haya: "Tutaifanya Marekani kuwa na nguvu zaidi, tutaifanya Marekani kuwa nchi tajiri zaidi, tutaifanya Marekani kurudi kuwa na sifa zake, tutaifanya Marekani kurudi kuwa na usalama wake. Kuifanya upya Marekani kuwa na nguvu “Make America great again”. Hii ilikuwa kauli mbiu ya kampeni yake.

Kabla ya kuapishwa kwa Donald Trump, Jaji wa Mahakama Kuu Clarence Thomas amemuapisha Mike Pence, mgombea mwenza wa Donald Trump, ambaye amekua rasmi makamu wa rais wa Marekani baada ya kuapishwa kwake.

Jackie Evancho, kijana wa miaka 16, amehitimisha sherehe hizo kwa kuimba wimbo wa taifa la Marekani.

Trump amechukua hatamu kutoka kwa Rais Barack Obama saa mbili usiku Afrika Mashariki. Amekula kiapo muda mfupi kabla ya saa mbili saa za Washington.