UFARANSA-KUARA ZA MCHUJO

Hamon na Valls kupambana katika duru ya pili ya kura za mchujo Ufaransa

Benoît Hamon (kushoto) na Manuel Valls (kulia), wagombea wawili walioshinda katika duru ya kwanza ya kura za mchujo kwa mrengo wa kushoto.
Benoît Hamon (kushoto) na Manuel Valls (kulia), wagombea wawili walioshinda katika duru ya kwanza ya kura za mchujo kwa mrengo wa kushoto. ©JOEL SAGET / AFP

Benoît Hamon na Manuel Valls watapambana katika duru ya pili ya kura za mchujo katika chama cha Kisoshalisti nchini Ufaransa Jumapili Januari 29, kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi ya durui ya kwanza ambao ulifanyika siku ya Jumapili Januari 22.

Matangazo ya kibiashara

Benoît Hamon na Manuel Valls wamepata kura ambazo zimewawezesha kuingia katika duru ya pili katika kura za mchujo kwa chama cha Kisohalisti nchini Ufaransa, alisema Jumapili jioni Januari 22 Thomas Clay, Mwenyekiti wa Taasisi Kuu ya kura za mchujo. idadi ya wapiga kura katika duru ya kwanza katika kura za mchujo kwa cham acha Kisoshalisti ilikua kati ya "miloni 1.5 na milioni 2, pengine karibu kufikia milioni 2," alisema.

"Wapiga kura wa mrengo wa kushoto, ninaamini kuwa walipiga kura kwa kutazama ujasiri wa mtu na sio kwa kumfahamu tu. Vinginevyo, hawangeweza kuniweka kwenye sehemu hii katika kura hizi za mchujo, " amesema Benoît Hamon, mgombea wa kutoka mrengo wa kushoto

Bw Hamon, mwenye umri wa miaka 49, alishinda duru ya kwanza kwa 36% akiwa mbele ya aliyekuwa Waziri Mkuu Manuel Valls mwenye umri wa miaka 54 ambaye alipata 31%. Katika hotuba yake, Benoît Hamon ameitaka timu yake inayoendesha kampeni kuzidisha uhamasishaji ili kupata ushindi Jumapili ijayo.

Kwa upande wake, Manuel Valls amesema anaamini kuwa atapata "ushindi" katika duru ya pili, huku akibaini kwamba Benoît Hamon atashindwa.