CHAD-UCHAGUZI-SIASA

Idriss Deby: uchaguzi wa wabunge waahirishwa kwa sababu za kifedha

Rais Idriss Deby amesema amechukua uamuzi wa kuahirisha uchaguzi wa wabunge kwa sababu nchi yake haina fedha kufanikisha zoezi hilo.
Rais Idriss Deby amesema amechukua uamuzi wa kuahirisha uchaguzi wa wabunge kwa sababu nchi yake haina fedha kufanikisha zoezi hilo. REUTERS/Alain Jocard/Pool

Rais wa Chad Idriss Deby kwa mara nyingine, ametangaza kuahirisha Uchaguzi wa wabunge uliokuwa umepangwa kufanyika mwaka 2015.

Matangazo ya kibiashara

Deby, amesema amechukua uamuzi huu kwa sababu nchi yake haina fedha kufanikisha zoezi hilo.

"Uchaguzi wa urais uligharimu pesa bilioni 52. Kuanguka kwa bei ya mafuta tulipata chini ya bilioni 30 ya pesa zilizoingia katika hazina ya serikali," amesema rais wa Chad wakati wa mkutano na vyombo vya habari.

Idriss Deby anafikiri kuwa gharama kubwa za uchaguzi zinasababisha kutofanyika kwa muda uliopangwa nchini Chad.

"Hatuwezi kuandaa uchaguzi mwaka 2017 au hata mwaka 2018. Uchaguzi unagharimu pesa nyingi," Idriss Deby ameongeza

Wakati huo huo, rais huyo ametaka kuwepo kwa mazungumzo ya kisiasa kati yake na vyama vya upinzani vilivyodai kura kuibiwa wakati wa uchaguzi wa urais mwezi Aprili mwaka uliopita.