SOMALIA-UCHAGUZI-SIASA

Mmoja kati ya wagombea katika uchaguzi wa urais Somalia ajiondoa

Wajumbe wa kutoka koo mbalimbali  nchini Somalia katika ufunguzi wa kikao cha Bunge la Katiba Julai 25 mjini Mogadishu.
Wajumbe wa kutoka koo mbalimbali nchini Somalia katika ufunguzi wa kikao cha Bunge la Katiba Julai 25 mjini Mogadishu. REUTERS/Ismail Taxta

Abdullahi Ali Hassan, mmoja kati ya wagombea 24 katika kinyang'anyiro cha urais nchini Somalia amejiondoa katika kinyang'anyiro hicho. amejiondoa kwenye kinyanganyiro cha urais nchini Somalia.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo ya Ali Hassan, inamaanisha kuwa sasa wagombea 23 ndio watakaowania nafasi hiyo wiki ijayo.

Abdullahi Ali Hassan amesema kuwa amejiondoa katika kinag'anyiro hicho baada ya kubaini kuwa, kuna wagombea wengi waontaka kuwa rais nchini humo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, wagombea hao wamekuwa wakizungumza na wabunge watakaopiga kura, kujipigia debe na kuwalezea sera zao.

Wagombea wote ni wanaume baada ya Faduma Dayib na Anab Dahir,wote wanawake kujiondoa mwaka uliopita.

Miongoni mwa wanasiasa wanaowania urais nchini humo ni rais wa sasa Hassan Sheikh Mohamoud, Waziri Mkuu Omar Abdirashid Sharmarke .