UTURUKI-SIASA

Kura ya maoni kupigwa Aprili 16 nchini Uturuki

Mageuzi ya kikatiba yaliyopendekezwa na Recep Tayyip Erdogan yataimarisha utawala wa rais wa Uturuki.
Mageuzi ya kikatiba yaliyopendekezwa na Recep Tayyip Erdogan yataimarisha utawala wa rais wa Uturuki. REUTERS/Brendan McDermid

Uturuki itaandaa kura ya maoni Aprili 16, 2017 ambayo itahusu mabadiliko ya katiba ili utawala wa rais kuchukua nafasi ya mfumo wa sasa wa Bunge. Mageuzi ambayo yamependekezwa na rais Recep Tayyip Erdogan.

Matangazo ya kibiashara

Jumamosi Februari 11, Baraza Kuu la Uchaguzi limethibitisha rasmi kwamba kura kuhusu mabadiliko ya katiba itafanyika tarehe 16 Aprili 2017,kwa lengo la kuimarisha madaraka ya rais Recep Erdogan. Katika hotuba yake iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Uchaguzi nchini Uturuki, Sadi Guven amesema kwamba tarehe hiyo imechukuliwa baada ya kuchapishwa kwa taarifa hiyo kwenye Gazeti Rasmi la Februari 11.

siku moja kabla,Recep Erdogan alisahihisha nakala hiyo inayolenga kuanzishwa kwa mfumo wa urais. Mageuzi hayai ni pamoja na kuruhusu mkuu wa nchi kuteua na kufukuza mawaziri, kutoa amri na kutangaza hali ya hatari. Katika kueleza uamuzi wake, Bw Erdogan amesema kuwa mabadiliko hayo ni muhimu ili kuipa Uturuki serikali yenye nguvu na imara, yenye uwezo wa kukabiliana na wimbi lisiyokuwa la kawaida la mashambulizi na matatizo ya kiuchumi.

Hata hivyo, nakala hii imezua wasiwasi kwa wapinzani na na mashirika yasio ya kiserikali ambayo yanamshutumu rais wa Uturuki kwenda kinyume na mamlaka yake, hasa tangu jaribio la mapinduzi la mwezi Julai 2016 lililofuatiwa na operesheni ya kamatakama na kuzua hali ya sintofahamu.