UTURUKI-SIASA-USALAMA

Washukiwa 330 wa jaribio la mapinduzi nchini Uturuki wasikilizwa

Kesi dhidi ya washukiwa 330 wanaotuhumiwa kujaribu kumpindua rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan imeanza Jumanne wiki hii jijini Ankara.

Rais wa Recep Tayyip Erdogan mjini Istanbul, Novemba 25, 2016.
Rais wa Recep Tayyip Erdogan mjini Istanbul, Novemba 25, 2016. Murat Cetinmuhurdar/Presidential Palace/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa washukiwa hao wataopatikana na kosa hilo watapewa kifungo cha maisha jela.

Tayari washukiwa hao zaidi ya mia mbili tayari wanazuiwa gereza.

Kesi hiyo imeanza katika Mahakama mpya, iliyojengwa kuwa na uwezo wa kuruhusu wafungwa zaidi ya elfu moja kuingia kusikiliza kesi dhidi yao.

Watu kadhaa walikamatwa baada ya kushindwa kwa jaribio hilo, huku wengine wakikimbilia nje ya nchi hiyo. Hata hivyo serikali ya Uturuki inaendelea kumshutumu mhubiri Fethullah Gulan kuhusika na jaribio hilo.