UFARANSA-URUSI-UCHAGUZI

François Hollande: twatakiwa kuwa makini kwa maandalizi ya uchaguzi

Rais wa Ufaransa François Hollande awataka Wafaransa kuwa makini na Urusi kwa madai ya kuingilia uchaguzi wa Ufaransa..
Rais wa Ufaransa François Hollande awataka Wafaransa kuwa makini na Urusi kwa madai ya kuingilia uchaguzi wa Ufaransa.. Television via REUTERS

Ikiwa imesalia miezi kadhaa kabla ya Uchaguzi Mkuu nchini Ufaransa, Rais wa Ufaransa François Hollande ametoa wito kwa uangalifu mkubwa kutokana na madai kuwa Urusi inalenga kuingilia Uchaguzi wa Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Madai kama haya yalitolewa pia wakati wa Uchaguzi wa Marekani lakini yakakanushwa na Moscow.

Katika hatua nyingine mgombea wa urais nchini Ufaransa kupitia chama cha Republican François Fillon amesema ataendelea na kampeni zake kutaka kuomba kura ili kuchaguiliwa kuwa kiongozi wa taifa hilo, hata baada ya Mahakama kuamuru kuchunguzwa kwake.

FrançoisFillon asema kuwa mashtaka dhidi yake yamefunguliwa kwa lengo la kumfanya asitishe nia yake ya kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.
FrançoisFillon asema kuwa mashtaka dhidi yake yamefunguliwa kwa lengo la kumfanya asitishe nia yake ya kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao. Philippe Wojazer/AFP/Getty Images

Mwanasiasa huyo anachunguzwa kwa madai kuwa wakati alipokuwa Mbunge alimlipa mkewe mshahara kwa kazi ambayo hakuifanya, madai ambayo ameyakanusha na kusema madai hayo yanalenga kumharibia jina.

Fillon mwenye umri wa miaka 62 na aliyewahi kuwa waziri mkuu, alikuwa anapewa nafasi ya kushinda uchaguzi mwanzoni tu mwa mwaka huu baada ya kuomba kupewa nafasi kwenye chama chake cha Republican mwezi Novemba mwaka jana.

Lakini toka wakati huo amekuwa akikumbwa na kashfa mfululizo kwamba alimlipa mke wake na watoto mshahara kwa kazi ambayo ilikuwa hewa kama wasaidizi wake wakati yuko bungeni.

Fillon amesema kuwa mashtaka dhidi yake yamefunguliwa kwa lengo la kumfanya asitishe nia yake ya kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.