Waziri Mkuu mpya wa Somalia aapishwa
Imechapishwa:
Waziri Mkuu mpya wa Somalia Hassan Ali Kheyre ameapishwa baada ya jina lake kupitishwa na wabunge nchini humo. Hayo yanajiri baada ya rais wa nchi hiyo Abdullahi Mohamed Farmajo kutawazwa wiki moja iliyopita.
Baada ya kuapishwa kwake, anatarajiwa kuliteua Baraza lake la Mawaziri.
Wakati huo huo rais Mohamed Abdullahi Mohamed akitoa hotuba yake ya kwanza Bungeni, amesema maadui wakubwa wa Somalia ni ufisadi na kundi la kigaidi la Al Shabab.
Somalia ilimpata rais mpya hivi karibuni baada ya kupitishwa na wabunge.
Somalia inaendelea kukumbwa na mdororo wa kiusalama unaosababishwa kwa kiasi kikubwa na kundi la Al Shabab, ambalo linaonekana kuwa pingamizi kwa maendeleo ya taifa hilo.