UFARANSA-FILLON-SIASA

Fillon ajaribu kuonyesha kuwa atashinda uchaguzi

Maandalizi ya mkutano wa hadhara umekamilika kabla ya kuwasili kwa mgombea wa mrengo wa kulia katika uchaguzi wa urais, Francois Fillon, ambaye anakutana na wafuasi wake, Jumapili hii Machi 5, 2017 katika eneo la Trocadero katika mji wa Paris.
Maandalizi ya mkutano wa hadhara umekamilika kabla ya kuwasili kwa mgombea wa mrengo wa kulia katika uchaguzi wa urais, Francois Fillon, ambaye anakutana na wafuasi wake, Jumapili hii Machi 5, 2017 katika eneo la Trocadero katika mji wa Paris. GEOFFROY VAN DER HASSELT / AFP

François Fillon anakutana na wafuasi wake katika eneo la Trocadero katika mji wa Paris kuanzia 15h (saa za Paris). Mkutano huo wa hadhara unafanyika mjini Paris, katika jaribio la mwisho, kuonesha kuwa uchunguzi kuhusu uhalifu, anaokabili, hautomzuwia kushinda katika uchaguzi wa rais.

Matangazo ya kibiashara

François Fillon anafanya mkutano wake huo Jumapili hii. Ili aweze kukabiliana na shinikizo ya viongozi wa kambi yake ambao wanataka kumshinikiza ajiuzulu katika kinyang'anyiro hicho, anahitaji kufanya mkutano kabambe katika eneo la Place du Trocadero. Lengo ni kukusanya takriban watu 50 000.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter, Bw Fillon amesema :"wanadhani niko peke yangu, wanataka niwe peke yangu, je niko peke yangu?"

Mabasi yamekodeshwa ili kuwasafirisha wafuasi kutoka mikoani hadi katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, ambapo kunafanyika mkutano huo. Jana, Patrick Stefanini, Meneja wa kampeni Francois Fillon aliyejiuzulu, ambaye atajiuzulu rasmi kwenye nafasi yake baada ya mkutano wa hadhara, alisema kuwa watu 15,000 walikua tayari kuorodheshwa. Yote hayo yatategemea na uhamasishaji.

Kura za maoni zinaonyesha, kuwa asilimia 70 ya wapigaji kura, wanataka atoke katika mashindano.

Viongozi wa chama chake watakutana kesho, kuamua hatima yake.

Mafanikio ya uhamasishaji pia yatategemea na uwezo wa waandaaji ili kuepuka kuzuka kwa hali ya sintofahamu na kufanya kilio chini ya uwezo wao ili mkutano huousgeuki kuwa maandamano dhidi ya majaji kama jinsi ilivyotokea hapo awali.