UFARANSA-FILLON-SIASA

François Fillon katika mkutano wa hadhara Trocadero: Naomba radhi

Mkutano wa hadhara wa François Fillon katika eneo la Trocadero Jumapili, Machi 5, 2017.
Mkutano wa hadhara wa François Fillon katika eneo la Trocadero Jumapili, Machi 5, 2017. Jacques DEMARTHON / AFP

François Fillon amekutana na wafuasi wake katika eneo la Trocadero Jumapili hii Machi 5 kuanzia 9 alaasiri (saa za Paris). Mkutano huo wa hadhara umefanyika mjini Paris, katika jaribio la mwisho, kuonesha kuwa uchunguzi kuhusu uhalifu, anaomkabili, hautomzuwia kushinda katika uchaguzi wa rais.

Matangazo ya kibiashara

François Fillon anafanya mkutano wake huo Jumapili hii. Ili aweze kukabiliana na shinikizo ya viongozi wa kambi yake ambao wanataka kumshinikiza ajiuzulu katika kinyang'anyiro hicho, anahitaji kufanya mkutano kabambe katika eneo la Place du Trocadero. Lengo ni kukusanya takriban watu 50 000.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter, Bw Fillon amesema :"wanadhani niko peke yangu, wanataka niwe peke yangu, je niko peke yangu?"

Mabasi yamekodeshwa ili kuwasafirisha wafuasi kutoka mikoani hadi katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, ambapo kunafanyika mkutano huo. Jana, Patrick Stefanini, Meneja wa kampeni Francois Fillon aliyejiuzulu, ambaye atajiuzulu rasmi kwenye nafasi yake baada ya mkutano wa hadhara, alisema kuwa watu 15,000 walikua tayari kuorodheshwa. Yote hayo yatategemea na uhamasishaji.

Kura za maoni zinaonyesha, kuwa asilimia 70 ya wapigaji kura, wanataka atoke katika mashindano.

Viongozi wa chama chake watakutana kesho, kuamua hatima yake.

Mafanikio ya uhamasishaji pia yatategemea na uwezo wa waandaaji ili kuepuka kuzuka kwa hali ya sintofahamu na kufanya kilio chini ya uwezo wao ili mkutano huousgeuki kuwa maandamano dhidi ya majaji kama jinsi ilivyotokea hapo awali.